

Lugha Nyingine
Shilingi ya Kenya yaporomoka dhidi ya dola?kwenye kiwango cha chini zaidi katika historia
Shilingi ya Kenya imeporomoka dhidi ya dola moja ya Marekani kwenye kiwango cha chini zaidi katika historia cha Ksh 150, na kuongeza shinikizo katika kupungua kwa akiba ya fedha za kigeni nchini humo jambo ambalo linafanya uagizaji bidhaa kuwa wa gharama za juu zaidi kufuatia ongezeko la mfumuko wa bei.
Benki Kuu ya Kenya (CBK) iliuza dola moja kwa shilingi 149.94 siku ya Jumatatu, ikipungua kwa asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Akiba ya fedha za kigeni siku ya tarehe 19, Oktoba ilifikia kiwango cha chini zaidi cha dola za Kimarekani bilioni 6.83, ambazo zilikuwa zinatosha kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi 3.67, ikishuka kutoka dola bilioni 7.29 mwaka mmoja uliopita.
Benki hiyo kuu, katika ripoti yake mpya iliyotolewa Oktoba 15 ya uthabiti wa sekta ya fedha, ililaumu kudhoofika kwa sarafu ya nchi hiyo kutokana na "kuimarika kwa kasi kwa sera ya fedha katika nchi zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi, zikilazimisha viwango vya riba vya kimataifa kupanda, na kusababisha wawekezaji kukimbilia sarafu zenye ubora kama dola."
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma