

Lugha Nyingine
Rais wa Jamhuri ya Kongo azindua majengo pacha ya ghorofa yaliyojengwa na kampuni ya China
Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa majengo pacha ya ghorofa yaliyojengwa na kampuni ya China huko Mpila, mashariki mwa Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, Oktoba 23, 2023. (Ubalozi wa China nchini Jamhuri ya Kongo/Xinhua)
BRAZZAVILLE - Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso amezindua majengo pacha ya ghorofa ambayo yamejengwa huko Mpila, mashariki mwa Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa miundo mbinu wa Jamhuri ya Kongo Bw. Jean-Jacques Bouya, amesema majengo hayo pacha ya ghorofa, yaliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Beijing (BCEG), ambayo ni kampuni ya China, ni "ishara kubwa kwa maendeleo ya utalii."
Meya wa Mji wa Brazzaville Bw. Dieudonne Bansimba, amekaribisha kuwepo kwa majengo hayo ya kifahari yaliyojengwa kwenye ufukwe wa Mto Kongo. Kisha akawaalika watu wa Kongo kuchukua umiliki wa majengo hayo mawili, ambayo kwa mujibu wake, yatachangia kupendezesha mji wa Brazzaville.
Yakiwa yamejengwa kwenye ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 121,800, majengo hayo pacha yenye ghorofa 30 na urefu wa mita 135, yatatumika kama kituo cha kibiashara. Moja ya majengo hayo litakuwa maalum kwa ajili ya ofisi, wakati lingine lina hoteli ya nyota tano.
Mradi huo uliohusisha mafundi wapatao 800 wa Jamhuri ya Kongo na China, umegharamia na Jamhuri ya Kongo na Benki ya Uuzaji na Uagizaji wa Bidhaa ya China, (Exim-China).
"Ninapenda kuwapongeza mameneja, wahandisi na wafanyakazi wa kampuni ambao wamefanya kazi hii nzuri ambayo inaashiria nguvu na uzuri, na inatoa ishara kubwa juu ya mustakabali wa uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Kongo," alisema Rais wa Jamhuri ya Kongo alipotembelea eneo la mradi huo Mwezi Septemba 2023.
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma