

Lugha Nyingine
Msafara wa pili wa malori yaliyobeba misaada yafanya safari kuelekea Gaza kupitia kivuko cha Rafah
![]() |
Lori lililopakia misaada ya kibinadamu likijiandaa kuingia Gaza katika kivuko cha mpaka cha Rafah upande wa Misri Oktoba 22, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa) |
RAFAH - Wafanyakazi wa kibinadamu wa Misri katika mpaka kati ya Misri na Gaza upande wa Palestina wamesema msafara wa malori 17 yaliyobeba misaada ya kibinadamu yamefika kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah upande wa Misri siku ya Jumapili, kabla ya kuelekea katika Ukanda wa Gaza uliodhibitiwa na Israel ambao unakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel.
Huo ni msafara wa pili wa misaada kutumwa Gaza baada ya msafara wa kwanza wa malori 20 yaliyobeba vifaa vya kibinadamu kuingia katika eneo la pwani siku ya Jumamosi.
“Msaada huo wa Jumapili unajumuisha chakula, vifaa tiba, maji, blanketi, nguo, sanda na vitu vingine” Ra'ed el-Gebaly, mfanyakazi wa kujitolea katika Akiba ya Chakula ya Misri, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua akiwa kwenye kivuko cha upande wa Misri.
Malori hayo ambayo yametayarishwa na Muungano wa Taifa wa Kazi ya Maendeleo ya Kiraia, ambao ni shirika lisilo la kiserikali (NGOs) ya Misri, kwa uratibu na Shirika la Hilali Nyekundu la Misri, yanatarajiwa kukabidhiwa kwa mfanyakazi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina, na Shirika la Msalaba Mwekundu katika upande wa Gaza, watoa misaada wa kujitolea wamesema.
"Utoaji wa misaada bado ni mdogo sana kuliko inavyohitajika kwa watu milioni kadhaa waliodhibitiwa huko Gaza ambao wanakosa mahitaji ya kimsingi chini ya hali ngumu sana," Abdel-Rahman Habat, meneja wa kitengo cha mahitaji ya msingi katika Mfuko wa Life Makers wenye makao yake makuu mjini Cairo, ambayo ni sehemu ya Muungano wa Taifa wa Kazi ya Maendeleo ya Kiraia amesema.
"Tunajaribu kuchangia kupunguza mateso ya watu wa Gaza na tutaendelea kufanya hivyo hadi mengi kati ya mahitaji yao kutosheleza," ameongeza.
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
Bahari ya Maua ya Mlima Jing katika Mji wa Hangzhou wa Zhejiang, China yakaribisha watalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma