

Lugha Nyingine
Ushirikiano kati ya China na Eritrea chini ya BRI ni muhimu kwa maendeleo ya baadaye: Mtaalam
ASMARA - Mchambuzi wa utafiti katika Kituo cha Masomo ya Kimkakati cha Eritrea, Bwana Fikrejesus Amahazion, amesema ushirikiano kati ya China na Eritrea chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) ni muhimu kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya viwanda na kufanya uchumi wa nchi hiyo uwe wa sekya mbalimbali. Bwana Amahazion amesema hayo hivi karibuni kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua, na kuongeza kuwa BRI imepata umaarufu duniani tangu ilipopendekezwa Mwaka 2013.
China imesaini mikataba zaidi ya 230 ya ushirikiano wa BRI na nchi zaidi ya 150 na mashirika 30 ya kimataifa.
Mwezi Novemba 2021, Eritrea ilisaini kumbukumbu ya maelewano (MoU) na China kujiunga na BRI huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukikua.
"Kwa Eritrea, tunaweza kufikiri kwamba pendekezo hilo litahimiza maendeleo ya viwanda na kuwezesha uchumi wa nchi kuwa mseto. Sote tunajua kwamba China imepata maendeleo makubwa katika kipindi cha muda mfupi, na hiyo ni nzuri sana kwa Eritrea kujiunga na pendekezo hili na kujifunza kutokana uzoefu huo," Amahazion amesema.
Mtaalamu huyo wa Eritrea amesisitiza ushirikiano wa BRI wenye manufaa kwa pande zote na matokeo yake chanya.
"Kwa China, Eritrea inatoa raslimali nyingi na ina watu wanaofanya kazi kwa bidii, na kuna uwezekano mkubwa sana ambao haujatumika katika nchi hii," Amahazion amesema.
"Maeneo ya ushirikiano ni kilimo, elimu, afya na mawasiliano kati ya watu. Tuna jukwaa thabiti la ushirikiano, lakini sasa tunatazamia ushiriki zaidi na maeneo yenye fursa zaidi ya ushirikiano katika kipindi hiki ambapo makubaliano ya kushiriki kwenye pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya China na Eritrea yanakaribia kutimiza mwaka mmoja na nusu tangu kusainiwa”. Ameongeza.
Mtaalamu huyo pia ameeleza matumaini yake kuwa ushirikiano na China chini ya BRI utachochea zaidi maendeleo ya Eritrea.
"Kuendeleza uwezo wa nguvu kazi ni moja ya maeneo ambayo Eritrea inatarajia kuyaimarisha," amesema, huku akiongeza kuwa miundombinu ni lengo lingine la msingi la ushirikiano na China chini ya mpango wa BRI.
Mtaalamu huyo pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya China na Afrika.
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
Bahari ya Maua ya Mlima Jing katika Mji wa Hangzhou wa Zhejiang, China yakaribisha watalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma